ARTICLE KUTOKA RAIA MWEMA IMEANDIKWA NA
24 Aug 2011
Toleo na 200 RAIA MWEMA
- Ni ule uzalishwao kwa makaa ya mawe
- Ni rahisi zaidi kuliko wa majenereta
- Wataalamu waishangaa serikali kung’ang’ania majenerata
- Uwezo mdogo msongo wa taifa watajwa kuwa kikwazo
TANZANIA inahitaji kuwekeza shilingi takribani bilioni 500 tu kuimarisha njia ya usafirishaji umeme (Gridi ya Taifa) ili iweze kubeba umeme mwingi zaidi utakaozalishwa na vyanzo vilivyoko kusini mwa nchi vinavyokadiriwa kuzalisha umeme wa MW1800 kabla 2016.
Wataalamu mbalimbali wa nishati ya umeme wameiambia Raia Mwema kwamba kwa kuwekeza katika miradi hiyo tatizo la umeme linaweza kuwa limeondoka ndani ya miaka mitatu kwa kutumia rasilimali za makaa ya mawe zilizoko kwenye Ukanda wa Maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor).
Pamoja na rasilimali hizo za makaa ya mawe yaliyoko Mchuchuma, Ngaka, Kiwira, zipo fursa nyingine tena za kuzalisha umeme wenye gharama ndogo zikiwemo zile za mradi wa umeme wa Upepo mkoani Singida na mradi wa umeme unaozalishwa kwa kutumia joto la ardhini (geothermal).
Vyanzo vya uhakika kutoka Wizara za Viwanda na Nishati na Madini vinabainisha kwamba uendelezaji miradi ya makaa ya mawe ya Ngaka Kusini, Mchuchuma na Kiwira utawezesha kujenga msingi wa umeme wa uhakika nchini kwa kuzalisha MW1200 ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2011.
Pamoja na kujenga msingi wa nishati hiyo ya nchini, umeme unaozalishwa kwa kutumia makaa ya mawe ni rahisi zaidi ikilinganishwa na vyanzo vingine kama vile mitambo inayotumia mafuta.
Viwango vilivyotolewa hivi karibuni na kuwasilishwa kwenye vikao mbalimbali vya majadiliano likiwamo Baraza la Mawaziri na vile vya Wabunge, vinaonyesha kwamba umeme wa makaa ya mawe utauzwa kwa senti 12 tu za Kimarekani, upepo senti 13 hadi 14, gesi senti 14, mafuta mazito (HFO) senti 20 hadi 22 na dizeli senti 30 hadi 33.
Kinachowaumiza zaidi wataalamu hao ni hatua ya Serikali kung’ang’ania miradi ya umeme wa dharura inayotumia mafuta ambayo ni ghali na kutoa umuhimu mdogo kwa miradi yenye kuzalisha umeme wenye gharama ndogo kama vile makaa ya mawe na upepo.
Wakati mradi wa Ngaka Kusini umekadiriwa kuzalisha MW400, upo pia ule wa Mchuchuma unaotarajiwa kuanza kwa kuzalisha MW600. Umeme kutoka Mchuchuma ndio utakaotumika kuendeza mradi wa chuma Liganga unaoaminika na wataalamu wa uchumi nchini kuwa nguzo kuu ya uchumi wa Taifa kutokana na umuhimu wa chuma katika kuendeleza viwanda na upatikanaji wa madini yenye thamani zaidi ya chuma chenyewe.
Katika hotuba yake ya Bajeti, Agosti mwaka huu, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, alielezea umuhimu wa mradi wa chuma cha Liganga kwamba yatapatikana madini adimu ya vanadium na titanium yenye thamani kubwa zaidi ya chuma.
“Kwa mfano, kiasi cha mashapo kinachotoa tani moja ya chuma inayouzwa katika soko la dunia kwa dola za Kimarekani 600, pia kinatoa madini hayo ya vanadium na titanium yenye thamani ya dola za Kimarekani 882,” anasema Dk. Chami katika hotuba yake ya Bajeti ya mwaka huu.
Kwa mujibu wa hotuba ya Dk. Chami, utekelezaji wa miradi hii ambao utakwenda sambamba na uhakiki wa makaa ya mawe, uchorongaji na upembuzi yakinifu kwa mradi wa chuma unatarajiwa kuanza mwaka 2011/2012 baada ya majadiliano ya mkataba wa ubia kukamilishwa na mkataba kusainiwa, ambapo dola bilioni tatu za Kimarekani zitawekezwa na mwekezaji katika miradi hiyo ya chuma na makaa ya mawe kwa mfumo unganishi.
Wataalamu wa madini wanaenda mbali zaidi kwa kubainisha kwamba pamoja na umeme, miradi hiyo ya makaa ya mawe itazalisha vile vile mafuta ya dizeli, mbolea aina za urea na sulphur.
“Wenzetu wanaita feature bread, pale unapata mafuta ya dizeli, urea, sulphur, tena kwa kilimo kwanza ndio mwelekeo sahihi, Afrika Kusini walifanya hivyo wakati ule wa embargo, China wanafanya hivyo, Australia wanafanya hivyo, makaa ya mawe ni mali, tena haya ya kwetu yana high quality,” anasema mtaalamu wa madini aliyezungumza na Raia Mwema.
Mbali ya gharama, umeme kutokana na makaa ya mawe ndio wenye kutegemewa zaidi na mataifa duniani (base load) ambapo takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa makaa ya mawe yanachangia asilimia 41 ya umeme unaozalishwa duniani, maji asilimia 16, gesi asilimia 20, nyukilia asilimia 15 na mafuta asilimia sita.;
Miongoni mwa wategemezi wakubwa wa umeme uzalishwao kwa makaa ya mawe duniani ni pamoja na Afrika Kusini asilimia 93, Poland asilimia 92, China asilimia 79, Australia asilimia 77, Kazakhstan asilimia 70, India asilimia 69, Israel asilimia 63, Jamhuri ya Czech asilimia 60, Morocco asilimia 55, Ugiriki asilimia 52, Marekani asilimia 49 na Ujerumani asilimia 46.
Hata hivyo, katika hali inayowashangaza watalaamu wa nishati na madini nchini ni wabunge kutoka Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho tawala, kutouona umuhimu wa miradi hiyo, na duru za bungeni Dodoma zinabainisha kuwa wabunge watatu, Zitto Kabwe, John Mnyika na Godfrey Lema, wote wakiwa kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndio wenye kutajwa kuwa wanashikilia bango la miradi hiyo ya umeme wa makaa ya mawe.
Miundombinu ya kusafirisha umeme
Hata hivyo tatizo la msingi linalotajwa na watalaamu hao ni uwezo mdogo wa miundombinu ya kusafirishia umeme na kwamba uwezo wa miundombinu iliyopo hautaweza kusafirisha umeme utakaozalishwa Mchuchuma, Ngaka na Kiwira na kwamba Serikali inawajibika kuongeza uwezo wa miundombinu hiyo kufikia uwezo wa KV400.
Wanasema kinachotakiwa ni serikali kutoa tamko la kujenga miundombinu ya kusafirishia umeme nchini kazi ambayo itachukua si zaidi ya mwaka mmoja huku uwekezaji kwenye miradi ya uzalishaji umeme ukifanywa na wabia.
“Kama unawapa TANESCO zaidi ya trilioni moja kwa ajili ya umeme wa dharura, kwa nini usitoe shilingi bilioni 500 tu kujenga miundombinu kwa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kuweka msingi wa nishati ya umeme kwa ajili ya maendeleo ya Taifa,” anahoji mtaalamu mmoja wa nishati na madini nchini.
Gharama za uwekezaji katika miradi hiyo ya uzalishaji umeme wa makaa ya mawe zinabebwa na wabia, na kwamba inachotakiwa kufanya Serikali kwa upande wake ni ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme zaidi ya MW1000 utakaozalishwa kutokana na vyanzo hivyo vya makaa ya mawe, upepo na joto ardhi (geothermal).
Tayari Kampuni ya Tancoal Energy Limited ambayo ni ya ubia wa Serikali kupitia NDC na Kampuni ya Intra Energy ya Australia wameanza uendelezaji wa mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka kwa ajili ya kuzalisha MW400 na wako tayari vile vile kuendeleza mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira na Kaburu wilayani Kyela wenye uwezo wa kuzalisha MW200.
Tayari soko la nje la umeme lipo ambapo katika MW200 zitakazozalishwa Kiwira zitauzwa pia nchi jirani ya Malawi.
Mradi mwingine unaosubiri utashi tu wa Serikali ni umeme wa upepo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida wenye uwezo wa kuzalisha MW300, ambapo wataanza na MW50 katika kipindi cha mwaka 2012/2013 kwa gharama ya dola za Kimarekani 136 ambazo zinatarajiwa kutolewa na Benki ya Exim nchini China.
Geothermal ni chanzo kingine cha umeme wa uhakika ambacho bado hakijaendelezwa kutokana tu na kutokuwapo utashi wa kisiasa, watalaamu wake waliandaliwa tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere kwenye miaka ya 1970 s na miongoni mwa maeneo yaliyothibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme huo ni pamoja na Songwe mkoani Mbeya.
Kyela kama kituo cha uzalishaji
Katika moja ya mapendekezo yake, NDC linaungalia mji wa Kyela mkoani Mbeya kama sehemu muhimu ya kuweka kituo cha uzalishaji umeme na bidhaa nyingine zitokanazo na makaa ya mawe.
Kituo kitakachojengwa Kyela kitaweza kutumika kuzalisha MW zote 1000 zilizokadiriwa kuzalishwa kutoka katika migodi ya Ngaka na Mchuchuma na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa na hilo linachukuliwa kuwa chaguo muhimu kutokana na ukweli kwamba kituo hicho kitatumia pia makaa ya mawe kutoka Kiwira.
Mapendekezo ya wataalamu hao ni kufanya mji huo wa Kyela kuwa kitovu cha viwanda vya kuzalisha bidhaa zitokanazo na makaa ya mawe kama umeme, mafuta ya dizeli, urea na sulphur.
Makaa ya mawe kutoka Mchuchuma na Ngaka yatasafirishwa kwa urahisi zaidi kwa matishari katika Ziwa Nyasa hadi Kyela.
Uzalishaji umeme nchini, kwa miaka mingi umekuwa ukitegemea zaidi maji na uhaba wake umekuwa chanzo cha mgawo wa umeme kutokana na ukame katika miaka ya 90, 2006 na 2009. Ni upungufu huo wa maji na hivyo umeme ulioisukuma Serikali kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji umeme na takribani wote wanatumia zaidi mitambo inayoendeshwa kwa mafuta hivyo kupandisha gharama za umeme maradufu.
Watalaamu wa madini na nishati ya umeme, hawaioni Tanzania yenye neema pasipo kuingia kwenye uwekezaji katika makaa ya mawe ili yazalishe umeme wa uhakika na bidhaa nyingine zinatokanazo na madini hayo. Wanahoji kunani kwenye miradi ya dharura ya majenereta.

0 comments:
Post a Comment