Fikra
Tunduizi _...Je ni kweli watanzania wanafanya mema kwa mambo ya kigeni
kwa kuwa yanapewa jicho la tatu na wageni ugenini na kukamatwa shati
ama kudondokea pua kwa mambo ya kwao?....sikia Hii 'Magazeti ya
Kiswahili ya Tanzania yanakosea zaidi katika uwasilishaji wa taarifa
kuliko magazeti ya kiingereza yanayofanya vyema sana. .Nanukuu 'Most
Kiswahili newspapers were generally sloppy in writing. . .on the other
hand English language papers performed wonderfully. (Print Media
Monitoring report jan to june 2012) . .usinijibu nashea tu! FYi
- Abdury Madiru and Mohamed Burhani like this.
- Madini Mazuri Ebo! Lazima tukujibu! Unategemea hiyo ripoti ya kiingereza ingesifia magazeti ya kiswahili? "mwamba ngozi huvutia kwake"! akili ya kawaida bila fikra tunduizi! @ Mwasalanga!
- Bro Mwaiteleke Johnson Hata kama Muamba Ngoma huvutia Kwake, lakin dhahiri mambo yanajionyesha, sikiliza Redio, angalia Runinga utaona haya yanayosemwa hapa, na ikiwa hawa wa Redio na Runinga wanaharibu, watashindwaje wa magazeti? Tatizo lipo kila mTz anaambiwa asipojua Kingeli basi hajafanikiwa, mbona Wachina wanakuja hawajui kiswahili wala Kingereza na wanabeba meno ya Tembo(wanafanikiwa adhma zao)?
- Dennis Mwasalanga @Madini na Jonhs. .ni ripoti ya kibongo tena inasema ukweli maana ni ya baraza la Habari Tanzania! Ingekuwa New york times sawa ni yakibantu hapa hapa sema imetumia International colonial ah samahan imetumia lugha ya neo co ltd!
- Bro Mwaiteleke Johnson Sasa kama baraza wao wanatumia lugha ya watu, unadhani magazeti yao yataweza kuwa thabiti kwenye kutumia Kiswahili?
- Madini Mazuri Mwasalanga, Johnson amenisaidia kufafanua! Amemaliza kila kitu nami nasema Amen Mwaiteleke! Mimi sikusema kuwa hiyo ripoti ni ya vyombo vya nje au ya New York times! Nimesema "ripoti ya kiingereza"
- Abdulrahman Salim Ali mi naona kwakuwa kuna magazeti mengi ya kiswahili yanazuka kila kukicha na ya kila namna na wasomaji ni wa mijini tu hvyo wanagombea wateja na kama ni hvyo kila mtu anataka kuwa tofauti na matokeo yake ni kuandika habari zisizofuata maadili ya uandishi na kuandika upuuzi na si kwamba ya kiingereza hayaandiki huo upuuzi ila ya kiswahili yamezidi na yanaangushwa na magazeti ya udaku, kwasababu kwenye kiingereza hakuna magazeti ya udaku TZ
- Abdulrahman Salim Ali mi naona kwakuwa kuna magazeti mengi ya kiswahili yanazuka kila kukicha na ya kila namna na wasomaji ni wa mijini tu hvyo wanagombea wateja na kama ni hvyo kila mtu anataka kuwa tofauti na matokeo yake ni kuandika habari zisizofuata maadili ya uandishi na kuandika upuuzi na si kwamba ya kiingereza hayaandiki huo upuuzi ila ya kiswahili yamezidi na yanaangushwa na magazeti ya udaku, kwasababu kwenye kiingereza hakuna magazeti ya udaku TZ na hyo ripoti kuandikwa kiingereza ni kwaajili ya kuwajulisha wafadhili tu.
- Madini Mazuri duh! Mwasalanga umezidisha kuchaipia! Fye, Fyo, Fyo!! Hizi hazipo! Kuna for your action (Fya) na for your information (Fyi)!
0 comments:
Post a Comment