"Wabunge Rudisheni Mkipatacho kwa Wananchi" Walio na Shida....

 Kwa namna ambavyo wabunge wanalalamika wakiwa Bungeni na kupaza sauti zao, kwa hoja zao  wanapata umaarufu mkubwa na tunawakubali, ilaa....haitoshi kukomea pale.

Ni wazi kuwa wapo wabunge ambao hata kama hatuwasikii wakitoa maneno buku kidogo "mjengoni Dom" , wana "show intergrity" na "respect" kwa jamii angalau kiasi fulani cha posho na Biz zao


Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu Tunaweza "proudly talk" kuwa amekuwa mfano wa Kuigwa kwa Kuwa mlezi wa Vituo 10 Vya kulelea Watoto Yatima kwenye Jimbo lake la Temeke, "Big up "Mbunge na Wabunge wote wangekuwa na "swaga" kama zako matatizo yote ya kijamii sanasana yatima, "watoto wanaoitwa wa mitaani" yoote yangekuwa "kwishnei"  katika jamii ya waTanga.....ah sorry  ya Watanzania.




Saidieni watoto..."Ningependa kuwaambia waheshimiwa wabunge wenzangu Tuwasaidie watoto wenye matatizo kama haya" (Yatima)..Ni kauli ya Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu wakati akikabidhi Watoto Yatima Msaada Wa Zaidi ya Milioni 7, Wilayani kwake katika Constituency yake pia. Agasti 08, 2012 Jumapili.

Maji Hufuata Channel yake.....

 
Hapa Chini Binti Mtoto wa Mtemvu Sitti Mtemvu akimpa Mkono miongoni  mwa walezi wa Vituo Vya Kulelea watoto Yatima, naa huyu binti anasoma "Abroad" ila ajapo Nchini na kile alichochuma huko anakuja kugawana na wakwao, lakini wabongo wengine wakienda majuu, wanachuma majanga ndo wanarudi kula na wakwao.... 




 


Na Hapa Chini Ni Sitti tena na Afisa mfawidhi wa kituo cha Taifa cha kulelea Yatima Cha Kurasini,Temeke-Dar es salaam, akipokea "GANJI" Kwaajili ya kituo chake...kiukweli Wanaoenda nje na kurudi na Majanga waige hapa kwa Kimwana huyoo wa Mtemvuanayesoma mahusiano ya Kimataifa nchini Marekani, wengine wakienda majuu wanarudi na magari na wanakuja kutupiga mizinga ya kununulia "wese la gari"


Iga mazuri, upate thwawabu, iga upuuzi upate laana....DM@2012

0 comments:

Post a Comment