HABARI ZAIDI KUPOROMOKA KWA JENGO POSTA DAR ES SALAAM


IJUMAA KUU 29.03.2013.......USIKU.


 Nimepita Eneo la tukio usiku..... MTAA WA INDIRAGANDHI ukiingilia Morogoro road POSTA  Dar es salaam NA kuona zoezi la uokozi likiendelea watu wengi sana na askari wengi wameimarisha ulinzi

Moja ya NUKUU ya SHUHUDA WA TUKIO NI kwamba "kuna moja ya mafundi amempigia Baba yake akiwa chini yaani akiwa amefukiwa na kifusi akisema AMEANZA KUKOSA HEWA......

Nukuu nyingine imesikika ikisema 
'" KIUKWELI VILE VINONDO NI VIDOGO SANA HAVIKUFAA KWA UJENZI KABISA YAANI VIDOGOooo"

Na Magari mengi ya wagonjwa yaani AMBULANCE YAPO PALE.....ASKARI WA KILA AINA NIMEWAONA PAMOJA NA MGAMBO Kuhakikisha usalama......



 TAARIFA ZAIDI NI KWAMBA....

Idadi kamili ya waliofikwa na mauti bado haijajulikana ila taarifa za awali ni zaidi ya 10
 

Ghorofa iliyodondokani liilikuwa bado katika ujenzi, chini kuna mafundi walikuwa wamepiga kambi wakiendelea na ujenzi.

Vikosi vya Waokoaji vinaendelea na shughuli ya kuwatafuta na kuwaokoa manusura usiku kucha.
Zaidi ya watu  arobaini wangali wamenaswa chini ya vifusi japo ni ngumu kujua idadi kamili ya waliofukiwa........na magari mengi yapo pale ya TRH yakiondosha kifusi kinachotolewa kwa makatapila

Miongoni mwa watu ambao wangali kupatikana ni wafanyakazi wa mjengo na watoto kutoka shule jirani ya mafunzo ya dini ya kiisilamu


Hadi naondoka eneo la TUKIO Watu wamejaa na uokozi unaendelea.....DUNIANI TUNAPITA JAPO KUTOFUATA VIWANGO VYA UBORA NI JAMBO LINALOGHARIMU MAISHA YA WATU WASIO NA HATIA.

Kuna TEJA mmoja eneo la tukio amesikika akisema "HUYO MHINDI NI LAZIMA AENDE JELA....... "


KAMANDA SULEIMANI KOVA NA JAMES MBATIA ENEO LA TUKIO



0 comments:

Post a Comment