No Kuchimba Dawa Policy yapewa "5" na wananchi, ila je inawezekana ama Tunataniana?

Being Serious Hakuna Steji muhimu kama ile unasafiri umebanwa halafu ndinga inapaki, unajiachia na ku do mambo yako kichakani...Alisema mkuu mmoja wa kitengo Tukiwa kazini


Sasa Baadhi ya wananchi wameniambia mimi Dennis kuwa mpango wa Serikali kupitia kwa Bro Harrison Mwakyembe mnamo Agosti 02 akiwa Mjengoni Idodomya,  kupiga marufuku kufanya hako kaanasa ka kuchimba Msituni Eti katawagharimu baadhi ya watu


Kiukweli Inakera kuchimba, ila ni kastarehe " kaukweli sana".....kuna kampuni moja ya simu ilikuwa na ka "advert" ka kastama wao mmoja anachimba halafu anaachwa kisha anagonga simu bus linamrudia...Hiyo yote ni raha ya kuchimba


Sasa Fuatana na haka kastori hapa chini na sasa Tunachange mood to seriousness




Baadhi ya "washkaji" wa pale ubungo yaani marafiki wa usafirishaji na abiria  wameipokea kwa wasiwasi kauli ya serikali kuwapiga marufuku madereva kuwaruhusu wasafiri kujisaidia maeneo ambayo hayana huduma ya vyoo

Safari za masafa marefu ni lazima uchimbe "nkota" kwa kibantu cha nyanda za juu kusini....ila sasa uchimbaji katikaspecific place hauna mvuto japo wadau wanasema kuwa Kuchimba porini kuna hatari ya usalama, wanyama, uchafuzi wa mazingira ila ukweli ni kuwa njiani pia Hakuna Vyoo vya kutosha

Na kwa Mujibu wa Waziri wa uchukuzi Daktari Mwakyembe  serikali itawafutia leseni ya usafirishaji wamiliki wa mabasi ambayo madereva wake wataruhusu ama kuwaacha abiria wao wachimbe kwenye  "unregistered zones"  kuanzia Oktoba mwaka huu....Sijui wenye matumbo msala ama "kulakula" itakuwaje?

Hata hivyo unafahamu kuwa mabasi mengi  hayajafikia hatua ya kuwa  "selfu contained" yaani selfu kontena ndani kwa ndani a.k.a humo kwa humo....sasa itakuwaje? na hata yale mabasi ya ndani kwa ndani ni kuchimba ujumbe mfupi, huwezi kuchimba kitu cha ughakika...sasa tunafanyaje wajemeni? ...ni nukuu za wasafiri wakiwemo Yahya Omari, HASTON SANIEL, Athumani Miraji na Mama Francis ambaye alikuwa akisafiri kutoka Dsm to Dom.

Suala la kusimamisha magari njiani pia limetajwa kuwa chanzo cha ajali na hivyo kuhatarisha usalama wa abiria na hilo wadau wa usafirishaji abiria wanaona kuwa serikali haijapata ufumbuzi sahihi na kujua nini kinahitajika

" Sirikali "ilikuwa na mabo mengi ya kufuatilia kwanza na sio kushikilia bango starehe za watu, unajua wengine walikuwa wanainjoi kuchimba kwa mafungu, na wengine wanapenda muda huo koz wanapenda "ch...o" yaani kuwacheck watu wa tofauti na wao wakichimba hata kwa mbali yaani wengine wanasema waziri amewakosesha "full cllipped film"...walisema baadhi ya raia wema pale Ubungo.



Wengine wameona kuwa uamuzi  huo utasaidia kuwa chanzo cha mapato kwa vijiji kujenga vyoo kando ya barabara na kutoa huduma kwa malipo

Kwa kuhitimisha ni vema Sirikali ikajua kuwa bado hakuna  majibu ya uhakika katika kero nyingine za usafiri ukiwemo uwepo wa matairi yasiyokidhi viwango, "mataafiki" kuzingua , kero ya mwendokasi, uholela wa nauli, watu wa mizani kuzngua  pamoja na ubiovu wa miundombinu.

0 comments:

Post a Comment