TATIZO NI KUONA PASIPO KUTAMBUA AMA KUTAMBUA BILA KUONA



Ukiwa Mwananchi unayeumizwa na mengi yanayoendelea hapa nchini unaweza kubali kuwa hakika endapo Mungu angeamua kutoa adhabu pale pale mtu anapokwepa uwajibikaji, basi wengi wange ama kuumbuka na wachache wangebakia wakiishi kwa amani

Na kama hilo lingetokea hapa hii isingekuwa tena dunia ile tuliyonayo na kwangu mimi hii ni ndoto ya mchana inawezekana dunia na watu wake waliopewa dhamana ya kuitawala nadhani binadamu wamekengeuka sana na hawana aibu  hata kidogo

Busara imeliwa na kuchakachuliwa kiasi kuwa watenda mema wanashangawa . na kuna sehemu ukiwa muwajibikaji utaambiwa heee kwani wee mbona unajipendekeza umeahidiwa dunia ama?

Na bila shaka wapo wanaosema UTAJIJU hata wazazi wakiwaambia watoto wao wenye njaa MUTAJIJU........

Wengine wakisema wananchi mnalia umasikini? eeeh basi mutajiju...wengine wakiwa viongozi, wengine watumishi na wengine wanachi wasio na Dira....na sitashangaa kama siku moja kiongozi akaitisha mkutano na kutukana matusi ya nguoni kwakuwa kwa sasa TUNAONA BILA KUTAMBUA NA KUSIKIA BILA KUSIKILIZA NA WENGI "TUNAZINGUA" wanasema vijana.

kwa neno MOJA TUMEPOTEZA DIRA na tunakataa kuitafuta kwa kuwa sisi ni mapunguani sio wote ila "SISI"....Na kama hutaki kuwa moja ya mapunguanbi basi CHUKUA HATUA NA SI KUSEMA SEMA NA KUYEYA YEYA


Nani asiyefahamu kuwa hapo ulipo una mambo unayoyaweza na una mambo usiyoyaweza

Endapo utaaminiwa na kupewa mamlaka ya kufanya mambo unayoyaweza ni dhahiri kuwa utakuwa fanisi lakini ufanisi wako utakuwa na walakini kama hutathmini na kukubali kutathiminiwa na watu ama jamii inayokuzunguka.

Wengi wetu tunajua fika mambo tunayoyaweza ila maranyingi tunakubali kufanya hata tusiyoyaweza ama kwa kupenda sifa ama kwa kusukumwa na kufanya kabla ya kufikiri.

Inawezekana kabisa kuwa kila binadamu anaweza kuwa fanisi katika nyanja yake na kutafuta zaidi kuwa fanisi katika masuala mengine muhimu kwake

Sasa hapa kwetu nchini hapa hapa hii ndiyo tathmini ya sisi:

Tunajua kila kitu na hakuna  wa kutujulisha masuala mengine na ndio maana kila mtu anataka kuongea bila kusikiliza sasa kama kila mtu ni muongeaji na waongeaji wanaongea pumba basi sisi sote ni mambumbumbu

Waliopewa dhamana na kusema wanasema tu bila kumaanisha ama kuhesabu maneno wanayoyasema na kusema tu ili mradi wamesema basi huu ni ufyatu

Wenye uwezo hawapewi nafasi wanapewa nafasi wenye ndugu ama jamaa wenye nafasi

Uvumilivu wetu umeporomoka hata mtu akikukanyaga bahati mbaya unaamini amefanya makusudi

Waliopewa dhamana wanatawala kwa kanuni zao za mifukoni kwa kigezo cha kusimamia sheria

Wananchi wengi wanashindwa kutekeleza wajibu na kulaumu serikali hata kwa kutupa maganda ya vyakula barabarani

Na mwisho wananchi wanataka mabadiliko bila kujua wabadilike kuelekea wapi......ukikosa ukweli unaweza kuamini uongo kwakuwa msema ukweli anakuficha

Matajiri wanazidi kutajirika na masikini wanazidi kusikinika kwa sababu nyingi sana sana ni Uvivu wa kufikiri wa baadhi ya watu bila kujali una hadhi gani, kuishi kwa ndoto bila kuchukua hatua na kubwa kuliko yote -: kukosa uwajibikaji na hapa ndipo tunataka watu wenye uwezo wa kuongoza na uzalendo wa ukweli na je tutawapata wapi na tutawapataje? Kitendawili..........

AMKA MTANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!WAKE UP!!!!!LEMBUKA!!!!CHUKUA HATUA NA KUWA MZALENDO!!!!!!!!!!!!!TUWALAANI WOTE WENYE NIA MBAYA NA NCHI YETU ILA TUWALAANI WOTE WASIOWAJIBIKA!!!!!!!!!!!!

0 comments:

Post a Comment