"TCRA Hakikisheni Hamtuletei MAFEKI, Msituletee mafeki wapendeni watanzania..waheshimuni watanzania"
Ni kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi alivyoguswa na kukithiri kwa Bidhaa feki za simu sana sana na vifaa vingine vya mawasiliano.
Alikuwa anadadavua tathmini yake katika maadhimisho ya miaka 10 ya huduma za mawasiliano kwa TCRA.
"Katika kipindi Hiki cha maadhimisho ya miaka 10 iwe kipindi cha kufuta mafeki yote nchini, watanzania Tuna uwezo wa kumudu vifaa bora..Alisema Dakta, Mwalimu Nchimbi.
Pia Mama Nchimbi alesema "Haiwezekani Taifa likawa halina siri na hapa akahoji JE TCRA haiwezi kuzuia mawasiliano ya ajabu ajabu yanayoendelea na kufichua kila siri za watanzania hasa wakiwa na taarifa za siri
Pia mawasiliano ya kitapeli Mkuu wa Mkoa anasema naye amewahi kupigwa yaani kuibiwa kwa mtu kumpigia simu akamtaja mchungaji anayemheshimu kuwa anauguza mwanaye, akatuma pesa chap chap na punde akagundua katapeliwa. " Sikuwa na cha kufanya ila baada ya siku kadhaa tapeli yule akapiga simu akabadili jina...nikamstukia nikaweka ukuu wa mkoa pembeni na nikaanza kupambana, nikawa mkali ( nahisi mkuu hapa alimshushia maneno makali)
Akaenda mbali kwa waandishi kuwa " Haiwezekani kila kitu kikaenda kwa vyombo vya Habari kuwa wasidhani kuwa vyombo kama BBC AMA CNN Kila kitu cha taifa lao kinaanikwa tu kwenye vyombo vya habari.
Dr Rehema Nchimbi Mkuu wa Mkoa Dodoma. |
TCRA Kpamoja na mapungufu ya mawasiliano yaliyopo imejitahidi kuboresha mawasiliano na kwa sasa watumiaji wa simu za mikononi wanafikia zaidi ya asilimia 60 ya watanzania.
Na kumekuwa na ongezeko la Matumizi ya Habari kwa mtandao na kwa kutumia Sera ya TEHAMA na kwa sasa karibu mambo mengi yanayoendelea nchini watanzania wamepata fursa ya kupata habari kila mara hata kwa kutumia simu ya mkononi.
Dkt Maria Sasabo meneja wa TCRA Kanda ya kati (Kulia) kwenye amadhimisho ya miaka 10 ya huduma za mawasiliano (Dodoma Tanzania November 29, 2013.) |
0 comments:
Post a Comment