je wajua?

Mijadala ya watanzania inayotumia mawazo yasio na utafiti ni upuuzi na ukosefu wa busara kuisaidia nchi yetu ya amani na utulivu wa raia pamoja na wageni.

Katika siku za hivi karibuni hakuna mwananchi ambaye anahamu ya kujua mambo na hajasikia mjadala maarufu wa madai ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Wapo wanasiasa wengi ambao ndio chanzo kikubwa cha kuwepo kwa mjadala huo maalumu kwaajili ya kuisaidia nchi yetu ya wapenda haki na amani daima.

Tunawapongeza wanasiasa wote ambao wameshiriki kuibua mjadala huo kwa kuwafanya raia wa Tanzania kuwa washiriki wa mijadala ya msingi ili kuleta mabadiliko ya usawa katika siasa, ambayo ndio msingi wa ustawi wa jamii.

Wanadiplomasia hunena mtu ambaye hashiriki siasa ataishia kuongozwa na viongozi dhaifu. Kila raia ana haki ya kushiriki siasa kama ambavyo inabainishwa na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Lakini si kila lianzaishwalo na wanasiasa lipokelewe kisiasa na kutendeka kisiasa.

Wanasiasa waanzishapo mijadala kwa sababu zozote walizonazo ni busara kuifuatilia mijadala hiyo kwakuwa siasa ipo kwaajili ya kustawisha jamii lakini kama hatuwezi kufanyia utafiti kauli zao tutapotea na kuzama katika dimbwi la Tanzania ya waasisi wa propaganda.

Tangu mjadala huo uanze hazijasikika kamati makini kama zile za akina Nyalali na Kisanga ambazo zilikuwapo kipindi kile na kufanya tafiti mbalimbali kwa wananchi.

Wapi Syovate wapi REDET? ama wanasubiri uchaguzi ufike ndipo waingie tena siasani?. Inaaminika kuwa katika kuanzoshwa kisiasa inaleta haja ya kufanyia tafiti kauli za wanasiasa. Watanzania ni wepesi wa kuelewa mambo na hata kama hawajaelewa basi watajadili tu vile vile wasivoelewa kwa uelewa.

Hapo ndio tunasisitiza kuwa makini na kuchunguza kula kauli isemwayo.

0 comments:

Post a Comment