SIKU ZA KUJISAJILI KUPATA VITAMBULISHO ZAONGEZWA DAR ES SALAAM

Taarifa kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa kupitia Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Jacksoni Maimu Zimeongezwa siku Saba (7) hadi jumapili ijayo August 5, Ili wakazi wa Mkoani Dar es Salaam wajiandikishe na kukamilisha Taarifa zao

Hata Hivyo zipo sababu nyingi zilizoilazimu mamlaka ya vitambulisho kuongeza siku, mojawapo ni Watu wengi jijini wapo "bize" kupanga mistari ni kama adhabu kwani utaratibu huo kiukweli ni wa kizamani sana

Hayo ni maneno ya watu wengi ambao wamekuwa wakifika kujiandikisha

Kila la heri NIDA japo utaratibu utumikao kiukweli unakera.

2 comments:

  1. Utaratibu wa kujiandikisha haujatulia nadhani mambo ya kupanga mistari ni utaratibu wa zamani, kama waliopewa kazi na NIDA wangepita nyumba kwa nyumba na zoezi lingekuwa endelevu ama wangewatumia wajumbe kuwaandikisha watu, japo nina wasiwasi na wajumbe kama wangeweza kulipatia zoezi

    ReplyDelete
  2. NI JAMBO JEMA KWA NIDA KUONGEZA SIKU ZA KUANDIKISHA WAKAZI WA DAR ES SALAAM, KWA MAANA WIKI MBILI WALIZOTOA ZISINGETOSHA KUSAJILI WAKAZI WOTE WA JIJI HILI WANAOKADIRIWA KUFIKIA MILION 7 SASA. NINGEWAOMBA WAKAZI WA JIJI KUCHANGAMKA NA KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE KAMPENI HII ILI MALENGO MAZURI YA SERIKALI YETU KWA KUTUMIA VITAMBULISHO VYA UTAIFA VIWEZE KUFANIKIWA.

    ReplyDelete