Msilete Uhuni katika katiba wajemeni.....na Je Kufuatia Uhuni wa Wachache Miezi 18 je Inatosha Kupata Maoni ya Watanzania wote?

Swali hili limesheheni katika vichwa vya watu, japo wapo wahuni wachache wanapenda kuwaburuza wenzao kwa kuwaambia nini cha kusema

Kumwambia mtu cha kusema huenda kumesababishwa na mfumo mbovu wa kutokujitambua kwa wana wan chi hii wengi ambao wamejikuta wakisema wasichojua kukitetea

Wapo raia wema ambao wana nia njema na wanajua nini wana kitaka japo hawawezi kuweka katika Ibara, ama vifungu, na ndio maana Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba anasema kuwa katika zoezi la kukusanya maoni kila Mtizeediii aseme matam,anio yake na sio kusema kinachosemwa na wengine

Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya maoni ya kufanikisha katiba ya wananchi kabla ya mwaka 2015 Joseph Warioba na  Augustino Ramadhani


Na Hapo wapo wapuuzi wachache ambao wanadhani watanzania ni mambumbumbu asiojua kujieleza, huyo amepotea, watanzania wanajua mengi ila mfumo umewabana kutokujua kuwa wao ni muhimu

Wapo watiizeedi ambao wana vitu ila hawajui Kiswahili, je Tume inafanya nini katika hilo?

 Soma kwa umakini hapa….

Jaji Warioba amesema pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika zoezi la ukusanyaji wa maoni lakini wananchi wengi wamejitahidi kutoa maoni yao kwa lugha ya Kiswahili, kwa hivo kiluga sio sana.

Ipo idadi ndogo ya wananchi wasiojua Kiswahili na kuongea vernacular zao, na hapo ndipo vijana walioenda mjini na kurudi kijijini ama waliokwenda shule wanapotafutwa na kuwezesha zoezi


MSISITIZO:

Tume ya Warioba imeamuru mara kadhaa kuwa ni marufuku viongozi wa serikali kufika maeneo ambayo inakusanya maoni ya wananchi

Kwani kufanya hivyo kunaweza kuwatisha wananchi na kuogopa “kukuchana” kama wewe ni DC ama vinginevyo


Jaji Warioba na Baadhi ya wanatume hao wamekutana Jumanne Augost 14, kwenye makao makuu ya Tume hiyo DSM NA Katika mkutano huo ndani NA BARAZA LA HABARI MCT, masuala mbalimbali yamejadiliwa ikiwa ni pamoja na tathmini ya kazi ya kukusanya maoni katika mikoa minane ya awamu ya kwanza ambayo ni pwani, Dodoma, Manyara, Kagera, Shinyanga, Tanga, Kusini Unguja na Kusini Pemba.

Jumla ya mikutano 386 imeshafanyika katika mikoa minane na kati ya mikutano hiyo Tume ilifanya mikutano 8 na makundi maalumu yakiwemo taasisi za dini na vyombo vya ulinzi na usalama.

Takribani  188,679 walihudhuria mikutano ya tume ikiwa ni wastani wa watu 489 waliofika katika kila mkutano, hata hivyo tume imesema kuwa ni poa namna idadi kubwa vile inajitokeza kutoa maoni yao.

Jaji Joseph Warioba Akizungumza na Waandishi na kuwafunda pia Jumanne 14.08.2012

0 comments:

Post a Comment