Nani Ataweza kushawishi Kubomolewa kwa Sheria "BOMU" Kwa Vyombo Vya Habari?

Soma Nukuu Za Wadau wa habari kuhusu Tasnia ya habari hapa nchini
Saedy Kubenea kATIKA pRESS ...DAR ES SALAAM 02.08.2012


HALI HALISI'S SAEDY KUBENEA " Mwanahalisi mara zote zote haijawahi Kuandika habari zisizo za uongo....Akiwa LHRC 02.08.2012.....Baada ya Stori ile namba 304 kutoka Nilipigiwa simu na wahariri wenye Heshima zao kuwa Stori iliyoifanya serikali ilifungie gazeti ni Big stori inahitaji Tuzo na Ni moja ya stori kali za uchunguzi hapa nchini….Sasa kama Wahariri wenye uwezo wa kupima na wamesomea fani wanasema Stori safi..iweje waziri Ambaye hajasomea aseme si safi?...sasa Stori kama Stori taendelea kusimama na nitaendelea kufa kwa msimao huo kwamba stori ni thabiti na ilisimamia misingi ya uandishi wa Habari….na polisi walipaswa waanzie hapo….”




"Tumeona kuwa kufungiwa Kwa gazeti la Mwanahalisi Kunaonyesha dhahiri Nia ya serikali kuleta Hofu na Kuwanyamazisha wapigania haki za binadamu"..... ONESMO OLENGURUMWA Mratibu Mtandao Wa watetezi wa haki za Binadamu Tanzania
Tumerudi kinyume katika masuaLa ya kuzingatia haki.....Tupo nje ya mfumo wa haki....Tunaweza kuongea tunaweza kwenda mahakamani ...Sisi Hatuamini haki kuwa kamili kama kuna haki zinavunjwa Gazeti kaMa hili limefungiwa Sauti yetu imepungua...HAKI ZIPO HAKI HAZITOLEWI....BI HELEN KIJO BISIMBA-Mkurugenzi Mtendaji LHRC
"Tunapinga Vikali Kufungiwa kwa MWANAHALISI, mnamo 30 julai 2012 kwa muda usiojulikana kwa kutumia sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, sura 229...moja ya sheria mbovu na isiyo na misingi ya haki za binadamu.....ONESMO OLENGURUMWA.
"Tatizo sio kwamba Mwanahalisi imefungiwa, tatizo ni Kwamba  TUNA UTARATIBU NA MFUMO WA SHERIA  ZINAZOSIMAMIA VYOMBO VYA HABARI AMBAZO NI MBOVU..NI MBAYA...Haitoshi Kusema Mwanahalisi imefungiwa...Tupinge Sheria..Tusimamie mchakato wa kupata sheria mpya.....Wenye vyombo vya Habari na wahariri wajue hili ndilo jambo la kufanya...kama imetokea Kwa Mwanahalisi ipo siku itatokea kwa mwingine, sheria si ipo?.......KAJUBI MUKAJANGA (KATIBU MTENDAJI MEDIA COUNCIL OF TANZANIA)  02.08.2012 MCT.

0 comments:

Post a Comment