Habari Hii na Na Esterbella Malisa na Immaculate Kilulya
Leo 02.08.2012 Mchana, MAHAKAMA Kuu Kitengo Cha Kazi JIJINI DAR ES SALAMA imeamuru Walimu kurejea kazini Mara moja na Kutangaza kuwa Mgomo umekoma.
Mahakama inasema kuwa Chama Cha walimu Tanzania CWT kiweke bayana kuwa Mgomo kwishne na Rais wa CWT ambaye ndiye alitangaza mgomo atangaze kusitisha mgomno kupitia vyombo vya habari
Kumbuka mgomo ulianza Julai 30, mwaka huu.
Vile Vile Mahakama imeamua kuwa walimu walioshiriki katika mgomo huo wanatakiwa kuwalipa fidia wanafunzi kutokana na kukosa masomo kwa kipindi chote cha mgomo ambao umeitwa BATILI.
Mgomo huo ambao umetumia kifungu cha 80- kipengele cha (1) cha sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 umedaiwa kutofuata sheria kutokana na notisi ya masaa 48 iliyotolewa na CWT kwa serikali siku ya mapumziko hatua ambayo ni kinyume cha sheria.
Jaji wa Mahakama hiyo Sophia Wambura ndiye ametoa uamuzi huo
Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri uMEwakilishwa na Mawakili wawili ambao ni Wakili Mkuu wa Serikali Obadia Kameya na Pius Mboya huku upande wa CWT ukiwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea Gabriel Mnyelle.
RAIS WA CWT MWALIMU GRATIAN MUKOBA ANATARAJIWA KUKUTANA NA WAANDIHI WA HABARI AGOSTI 3 JIJINI DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment