Maneno ya Kaimu Katibu Mkuu Wa Wizara Ya elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ualimu Ndio Taaluma pekee Ambayo ukimaliza ama kuhitimu masomo yako Unaajiriwa Bila Kusota Nyumbani kama katika Taaaluma Nyingine ambazo unaweza kusona na kusugua 'benchi" hata miaka kadhaa bila kupata ajira.....Mfano ni uandishi wa Habari n.k.....
Na Kwa Niaba ya Serikali akasisitiza kuwa Bado kuna fursa za majadiliano na sio kuendeleza Migomo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi... |
Sasa Kwanini Walimu Mugome Huku mkijua Ninyi mpo katika Sekta ya upendeleo, mnapata mikopo, mna Direkt entry makazini so why walimu?? ........Swali Hili Limejibiwa pia na Rais wa CWT Gratian Mukoba kwamba "....Kumwajiri Mwajiriwa sio "Feva" ya mwajiriwa...na kuniajiri moja kwa moja haina maana ya kunyanyaswa....Kukataa kutupa chetu ni Kuminya Haki yetu....Sisi Tumesimama kuonyesha kuwa ni Watanzania Wanaojitambua.....
Serikali ilipoanzisha Mfumo wa Elime "MEM" ilijitahidi kuweka jitihada katika Vitabu na Madarasa na bila kukumbuka kuwa Ni Afadhali Kuwa na Mwalimu aliyeridhika usiwe na Vitabu, Kuliko kuwa na Mwalimu asiyeridhika na vitabu lukuki"...(Mukoba 01.08.2012 CWT Makao Makuu)
Pia Mukoba anasema Mwalimu anaweza kufundishia chini ya mtu watoto wakaelewa kuliko kuwa na madarasa mazuri halafu elimu empty....
Hatma ya yote nini?
Rais Mukoba anesema Serikali irudi katika akili zake, iweke bajeti Ya kutosha katika Elimu, akatolea mfano kuwa Wakati ilipoingiza Mfumo wa elimu kwa Wote ilichemka kutotenga bajeti ya asilimia 6 ya pato la Ndani yaani GDP, na akasema kwanini angalau Tusiige kwa Kenya ambayo imetenga 7% ya pato la taifa, Uganda 4.8%, Rwanda 5.8%, Burundi 3.8 na Tanzania inatenda 1.4% Tu ya pato lake la taifa na ndio maana kuna matatizo ya madawati, matatizo ya Mishahara na Madai Lukuki madai buku kichele, kwahivo Suluhisho kwa Mujibu wa Rais "SErikali irudi Katika Akili Zake"
Friendly to The Press is CWT's President Gratian Mukoba |
Naa Kwa waathirika Wakuu wa Mgomo Ma "Pupils" wameendelea "Kula Bata" Na kuinjoi "friidom of the frii souls" bila Kutetereka, maana wengine hawapendi kukaa nyumbani so lazima wende mashuleni mwao na Kupata free games and talks hapa na pale
Hapa tunapiga vikapu tu, nyie endeleeni na Migomo... |
Bora Kucheza Kiduku Hadi mgomo Utakapokata |
Na kwa Updates Leo Mahakam Kuu Kitengo Cha kazi itatoa Ruling kuwa Mgomo Ni Halali ama Sio Halali...stay blogged for moree updates....
Daa Kweli kazi ipo hapa duh duhh yaani wanafunzi kiduku, walimu Msimamo na Govt Siasa kama kawaaaa
ReplyDelete