Waafrika Tunatazamia nini Uchaguzi wa Niger?

 

Wana wa Niger watapiga kura 30 Januari 2011 kuchagua wabunge na rais wakati ambapo wagombea wanautaka utawala wa kijeshi wa nchi hiyo uibadili tume ya uchaguzi.


Mnamo mwezi wa Februari mwaka 2010, wanajeshi wa Niger  walitwaa madaraka kwa kumpindua Rais Mamadou Tanja, kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa anakusudia kufanya njama za kuibadili katiba ili  aongeze kipindi cha mamlaka yake ya urais.

Hali ilikuwa ya mvutano muda mfupi baada ya kumalizika  kampeni za uchaguzi.Wagombea urais wanane kati ya 10  wametishia kuususia uchaguzi huo ikiwa serikali ya kijeshi  haikuuakhirisha.

Wajumbe hao wamelalamika juu ya maandalizi mabaya ya uchaguzi wa majimbo. Hayo ameyasema pia aliyekuwa Waziri Mkuu Hama Amodou, mwenye matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika uchaguzi huo hapo kesho.

"Ikiwa uchaguzi wa bunge na wa rais utafanyika katika mazingira   kama yale ya uchaguzi wa  majimbo, basi tutakabiliwa na matatizo  makubwa." Amesema Amodou.

Lilikuwa jambo la kuvutia kumwona Amadou ghafla akiwa  pamoja na hasimu wake mkubwa wa kisiasa, chama cha MNSD kilichokuwa kinatawala nchini Niger.

Itakumbukwa kwamba chama hicho ndicho kilichomvua madaraka ya uwaziri mkuu, Amadou alipokuwa  katika serikali ya Rais Tanja. Amadou alikabiliwa na tuhuma  za  rushwa na alitiwa jela ambako sasa rais wa hapo awali. Tanja anatajwa pia kwenye tuhuma za rushwa.

Shabaha  ya  uchaguzi  huo  hapo  keshi nikurejesha  demokrasia nchini  Niger, baada ya  jeshi  kutwaa  madaraka mwezi  februari mwaka  jana.  Lakini  pana  utatanishi  juu ya   tume  ya  uchaguzi. Msemaji  wa   chama cha MDN  ameutaka  utawala  wa  kijeshi uibadili  tume hiyo. Msemaji huyo  Malam Sani  Mahamanne   ameeleza  kuwa tume hiyo ina sifa mbaya.Ameeleza  kuwa wagombea   wa  vyama vyote  kumi wametaka kuahirishwa uchaguzi huo.

Lakini wananchi  wa Niger   hawataki kuona mivutano  baina  ya  wanasiasa bali wanataka kuona matatizo  ya nchi yao yanatatuliwa. 

Niger inakabiliwa  na  vipindi vya  ukame mara  kwa  mara vinavyosababisha  njaa nchini.  Hali  ya  elimu  pia imo katika  hali mbaya .Maalfu ya   vijana  hawana  aira.

Wagombea   wote  wanatoa   ahadi zinazofanana.  Lakini   suala  la ugaidi halitiliwi maanani  miongoni  mwa wagombea-  yaani harakati  za  makundi yanayoyakiribia  alkaida   ambayo  mara kwa mara yamewateka nyara   watu kutoka Ulaya.

Hivi  karibuni   tu vijana  waliokuwa   na silaha  waliwateka nyara  wafaransa wawili katika  mji  mkuu Niamey.Magaidi  waliwaua wafaransa  hao baadae. Hatahivyo baadhi  ya wananchi wa Niger  wanasema  jambo muhimu  zaidi  ni  mchakato  wa  kurudisha demokrasia nchini  an  hivyo kuweza kuepusha hatari  ya  kuimarika wanaitikadi kali  wa  kiislamu.

Watu  karibu milioni saba   wanastahiki kupiga kura  hapo 30 january.  Wachunguzi wanatarajia kuona  uchaguzi huo  ukifanyika kwa  utulivu. Katika changuzi za nyuma vyama vyote  viliyakubali  matokeo ya uchaguzi  licha  ya  kasoro  fulani zilizojitokeza.
              
Habari hii imefanikishwa kwa rejea ya idhaa ya kiswahili ya dw/swahili.com

0 comments:

Post a Comment