Jicho Langu Likionacho Ni Cha Kutamausha Na Kuumiza Fikra ZANGU”…

UPDATED...19.08.2012 EID EL FITRI DAY

Me...I see Precipitations whenever i think of mai pipo

Jicho Langu Likionacho kinatamausha na Kuduwaza Fikra Zangu

dennismwasalanga@gmail.com

SikuKUU ya EID EL FITRI Nimeamua kufanya Kautafiti ka kiana tu katika maeneo kadhaa ya Jiji La Foleni, joto, makelele, Moshi wa Magari, fujo fujo, masista duu, masharo, mafukara pamoja na watu wengine wengi na majumba ya kutosha yaani jiji la Daslam.

Nimeanzia Kibaruani usiku...na kuelekea Ibadani kisha mjini na hatimaye Kurejea Nyumbani

Samahani
kama msomaji wangu utaona natumia lugha ngumu naamini utaelewa kwani haya mambo kila siku yanasemwa na Huenda lugha ikitumiwa kama nayotumia mimi labda tunaweza kuelewana wandugu wangu

Katika utafiti ambao nimetumia “Observatory methodi” yaani kushuhudia mwenyewe na sio kumuuliza mtu wala Kufanya Hojaji wala Kutumia Swali kwa karatasi

Kwanza katika mapambazuo kibaruani nimejiridhisha kuwa mambo nadhani yakawa safi sana japo sijui wateja wangu walionaje, hapa sitaki hoja sana kwani itatuondoa kwenye mantiki ya niandikacho

Baada ya kutoka Kibaruani nikaingia Kanisani nimeona namna watu walivyopendeza na wakisinzia wakati wa mahubiri, hata mimi pepo wa usingizi alitaka kuninyemelea ila kwa kuwa nilikuwa ibadani huku nafanya kauchunguzi kangu pepo akashindwa kulegea na kutokomea kabisaa na nikapata “Preechings” kwa uzuri kabisa…Mwenyezi Mungu anisaidie na kunisamehe endapo nimeteleza

Ilaa nalisikitishwa na namna ambavyo wengi walionekana katika mavazi ya aghali na mikononi mwao walikuwa na vijipesa vya “KOINI” vimeshikwa kisawasawa ili angalau visijedondoka na kufanya heshima iingie matobo

Baada ya hapo Nikaelekea kwenye “Muamala” yaani “ATM”  kushuhudia kama unasoma vyema, hiyo ni plan A” kwa  bahati mbaya aaahggrrrhhh!!! Mumala Haukusoma vema…nikatumia plan B, Maisha yanaenda vema, sasa Baada ya kutoka Muamalani nikaendelea na kupepesa macho katikati mwa jiji hili la Meck sadick

Eneo la Chuo Cha Biashara yaani CBE Nimeona watu wengi wakiwa katika Vazi la kanzu, na wakiwa wamezongwa na akina mama na watoto wadogo sijui kama ni watoto zao ama laaa…

…walikuwa wakiombaomba kiasi cha kunifanya niwashangae kwa sekunde kadhaa kwani kuna kitu walikuwa wanagombea na niliposogea nikabaini kuwa walikuwa wakigombea pesa, na ni pesa ambazo walipewa na wahisani katika maadhimisho ama kusheherekea siku ya Eid el Fitri ambao walikuwa wametoka ibadani.

Nalazimika kuwaita wahisani kwani wengi wao walikuwa ni “watanzania wenye asili ya ngozi nyeupe”

Nilipojiridhisha kuwa nimeona ya kutosha na nimekereka vya kutosha nikalazimika kuondoka pahala pale kwani roho iliniuma kwakuwa naamini ningekuwa serikalini ningetafuta namna ya kuwasaidia ninge… ninge… ninge…….japo siwezi nikawahakikikishia hilo…labda hata mimi “ningekuwa Kiongozi” labda namimi mijisenti yangu ningeipeleka kwenye akaunti uswisi kwaajili ya matumizi ya baadae wakati ndugu zangu wakiombaomba hapa nchini.

Hilo Tuliache, kwani wengi tunasema Ninge na tukipewa dhamna tunakuwa walewale kama wale ambao tunasema ni mapapa sijui manyangumi cjui wahujumu mi sielewi majina hayo ambayo yakiwekwa katika ubeti nadhani yataingiza albam nyingi za muziki sokoni na kuteka soko huku watayarishaji wakisota na na wachache waliokaa katika Production studios na wasambazaji “wakila bata” baada ya kuwachakachua watunzi wa beti hizo

Mbali na Hilo,  Baada ya hapo Nikakwea daladalani kurejea nyumbani, kwa nauli ya Shilingi mia tatu kutoka katikati ya jiji kuelekea ninapoishi, nikapita eneo Fulani la mataa na kumuona “mtanzania mwingine mwenye asili ya ngozi nyeupe” katika gari zuri linalofanana na lile analotembelea waziri mkubwa  aliyesemekana kuyapiga vita huku naye akiendelea kuyatumia
Hilo ni VX Land cruizer Limejaa jaa hivi nadhani ni la zaidi ya milioni100, mi sio mzuri katika kujua bei za magazi... new Modern mpya ambayo nadhani ni “automatic” kuanzia saiti mira hadi milango
Sasa jamaa huyo ambaye alikuwa anaendeshwa na Mtanzania mwenye asili ya "ngozi nyeusi"...huyu mtanzania mwingine sasa aliyeweka kishoka, mwenye asili ya ngozi nyeupe,  kwa “kono lake la mavi” akampatia mlemavu anayejisogeza kwa kujivuta “JERO” kwa kutumia kono la kushoto na tena huku akitazama mbele yaani hataki kumuona
Nilitamani niseme neno ila maneno yangu yalizikwa katika moyo wangu na daladala nililopanda likang’oa na kichwa kinazidi kuwa kizito kwa yote nilyoyaona.

wakati naelekea nyumbani yaani baada ya kuteremka daladalani hatua chache kuelekea Nyumbani kwangu, ninaendelea kufanya Kauchunguzi ka jamii yangu siku hii ya sikukuu, napita sehemu ambapo watu hununua maji ya bomba, namuona mtoto mdogo kati ya umri wa miaka mitatu na ushehe kwa makadirio

Mototo huyo akijaribu kufungua bomba bila mafanikio, na sikutaka kujua kwanini anafungua bomba kwani nilijiaminisha kuwa huenda ana kiu ya maji…nilipomtazama kwa uzuri aahh alikuwa amejisaidia huku nzi wakimfuata…oh lord tusaidie watanzania....na siku yangu hapo ikawa imejawa na huzuni kwani hakuna hata kimoja ambacho nimekifurahia, Nimeamua kukaa ndani tu kwani kila nitembeapo naona huruma kwa jamii yangu na sina cha kuwasaidia zaidi ya kuwaombea kwa Mungu. Amen.

Nawatakia siku njema, hayo nimeyaona mimi , wewe je? ............


0 comments:

Post a Comment