GARI "LACHUM" BAHARINI , KISA MASIHARA YA DEREVA!!

Asiyesikia la mkuu huvunjika hata meno ndivyo waweza sema, kwani hilo limemkuta mmiliki wa Gari la kifahari wakati akitaka kuingia katika PANTONI Akitaka kuwahi ndipo akakutwa na haraka haraka isiyo na baraka, baada ya gari lake kuingia maji chumvi kwa sababu ya kutozingatia usalama wa kwenye gati Kigamboni Jijini JULY 30,2012 ASUBUHI.

Kilichomkumba ni kwamba Kivuko Kiliruhusiwa kung'oa na kilishaanza kung'oa gati, yeye akajifanya ana upesi, ndio basi Chabo pics hizi hapa chini:




Baharia wa MV MAGOGONI (Kivuko cha Posta to Kigamboni) akitoa ufafanuzi kwa Mwandishi na kubwa amemlaumu dereva kutaka kuwahisha gari lake katika Pantoni(Ferry) ambalo lilikuwa limeshang'oa namnga, na hatimaye alivyoona kachemka akaruka na kuliacha gari liseerereke hadi baharini, likajipigiza katika Mlango wa Kivuko na kuchum ndani ya maji "chubwiii!!!!

Mmoja wa Baharia wa Kujitegemea LUCAS SENGEREMA Ni miongoni mwa waliolipoa gari baharini na Kubwa kijana ametoa pendekezo la kuwatimua wafanyakazi wote wakiwemo walinzi wote wasio na taaluma ya maji, yaani kuogelea na kuzamia kufanya uokozi, na kwa mujibu wa Baharia huyo asiye na ajira, haina maana kuwa na wafanyakazi wanaofanya kazi karibu na Bahari na ikitokea kama la gari kuzama wanabaki wakiduwaa na kushangaa
...more updates coming.......

1 comment: