JE Mwanamke wa Tanzania anafaidika vipi na siku ya Mwanamke wa Afrika?
Tanzania leo imeazimisha siku ya mwanawake wa kiafrika huku wanawake wengi wakiiona siku hiyo ya kisiasa zaidi
Siku hiyo maalumu ya kuwaenzi wanawake iliasisiwa july 31 mwaka 1962 hapa nchini
Siku hii inaazimishwa wakati wanawake wengi wa hapa nchini wakikabiliwa na changamoto nyingi hususani wale wanaofanya kazi mbalimbali katika maeneo ya mijini
Wapo akina mama mbalimbali ambao wao kwao kazi tu na hata hawatambui uwepo wa siku hii na kwa mujibu wao siku hiyo hata hawajui umuhimu wake na wameona bora kuendelea kupiga kazi maeneo yao
Wakati akina mama hao wakiendelea na shughuli zao na kukiri kutoitambua siku yao wenyewe, katika eneo la makumbusho ya taifa jijini hapa yanafanyika maadhimishi yaliyolenga kutuma ujumbe kwa watanzania na kubwa ikiwa wanaitazamaje sikuhii
Kongamano la siku ya mwanamke wa kiafrika limekuwa likizimisha kwa takriban mika 50 hapa nchini na katika mataifa mbalimbali barani Afrika kwa lengo la kutathmini maendeleo na vikwazo vyake kwa wanawake mijini na vijijini.
FURAHA Hii ya watoto wa kike hufifizwa kadri wakuavyo na siku kama ya leo tunapenda furaha hii itetewe na iendeleee kwa mwanamke wa AFRIKA |
0 comments:
Post a Comment