KWANINI WATANZANIA TUAMINI KATIKA MIGOMO?

MIGOMO!!! MIGOMO!!! MIGOMO !!!! MIGOMO!!!!!


Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania Gratian Mukoba Akitoa ufafanuzi wa azma yao ya kugoma kutokana na Kutofikiana muafaka na kamati ya upatanishi baina yao na mwajiri wao ambayo ni Serikali ya Jamuhuri ya Muungano katika makao makuu ya CWT Dar es salaam 28.07.2012...Picha na Esterbella Malisa.


Wakati CWT ikisisitiza ulazima wa kugoma ili kushinikiza kupewa stahiki yao (Ongezeko la mshahara kwa asilimia 100, posho, pamoja na stahiki ya kulipwa wakifanya kazi katika mazingira magumu) Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi kupitia Naibu waziri wake Philipo Mulugo, imeshikilia msimamo kuwa Mgomo ni Batili.

Na kwa mujibu wa Mulugo mwalimu yeyote ambaye hatafika kazini kuanzia jumatatu 30.07.2012 atakuwa amekiuka agizo la serikali na atahesabika kama mtoro.

 Siku ya Jumatatu yaani kesho (30.07.2012 Ndipo walimu wameema wataanza kugoma nchi nzima.


CWT inasema mgomo ni halali kutokana na usuluhishi kushindikana na kwa kuzingatia kifungu cha 80 (1) kifungu (d) cha Sheria ya ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, "walimu wanachama wa CWT walianza zoezi la kupiga kura kuidhhinisha mgomo Julai 25, mwaka huu na zoezi hilo likamalizika julai 27 Ijumaa, na kuungwa mkono kwa asilimia 95.7 ya wanachama wote, na hivyo Mgomo upo"...(Mukoba)

Tunaweza kuongea mengi ila ukweli utabaki kuwa palepale kwa serikali kuyatazama makundi mbalimbali katika uajiri wake, wengine wanakula "bata" wengine wanakula shuruti...Kama serikali ina nia ya kuondosha migomo ijitathmini upya na kuondoa ubepari miongoni mwa wafanyakazi wake, kwani wengine wanalipwa mamiliono na hawana kazi kubwa sana ya kufanya huku wengine wakilipwa "vijisenti" na wengine ndio kabisaa hata hawataki kusema.


Migomo sio suluhu ya matatizo, japo hushinikiza na kukumbusha wajibu, ni vema Serikali ikawa na meno na maamuzi sahihi, je ni kweli serikali haina pesa? Ni wazi kuwa pesa ipo ila mgawanyo sio sahihi, kama vipi wafanyakazi wa umma wapewe mishahara kutokana na kazi wafanyazo na uzalendo uwekwe mbele.








0 comments:

Post a Comment