Majibu Upupu ya Manesi Yanasababishwa na maisha Magumu

Wakati Bunge la Bajeti LIkiendelea kurindima Huko Dom, Bunge Hilo lililotaniwa ni Modern........Baadhi ya Wabunge wanasema kuwa Kumbe Madaktari na wauguzi wamekuwa na maneno makali na kuishiwa na Huruma kutokana na muda mrefu wa kufanya kazi pamoja na ugumu wa Maisha.

Lakini pia fuatilia Mazungumzo haya:

Doctor: Karibu
Mgonjwa: Aksante

Doctor: Habari Yako?
Mgonjwa: Salama

Doctor: Mzima?
Mgonjwa: Ndio Mzima

Doctor: Unasumbuliwa na Nini?
Mgonjwa: Kichwa

Doctor: Kinaumaje

Mgonjwa: Upande mmoja

Doctor: na nini Kingine?
Mgonjwa: Na mwili Mzima

Doctor: Umeanza lini?
Mgonjwa: Hata sikumbuki

Sasa hapo kwanini hao watetea haki wasichoke? maana maelezo hayo ilitakiwa yatoke kwa ujazo na yaeleweke lakini mgonjwa anasubiri aulizwe kila kitu na kama kweli unaumwa na unasema u mzima na badaye unaumwa sasa watanzania hapo ndo tunapokuwa wachemkaji.


Ona hayo mambo, umeenda kupima na unaumwa ila hadi kumweleza daktari unalepetalepeta tu badala ya kwenda moja kwa moja na kuyatoa maelezo yenye ujazo, hii pia inasababisha kuwachosha maafisa matibabu bila sababu, wakiwajibu upupu inakuwa balaa

Kwa mazingira Hayo unataraji wauguzi na Madaktari wasiwe na majibu ya fyongo?

Ila Kwa upande mwingine wauguzi wa sasa wanahitaji kuwa na wito zaidi kwani waTZ wote wameshachakachuliwa na lyf stlye.

0 comments:

Post a Comment