23.07.2012 MAMA PROFESA ANNA TIBAIJUKA AFANYA ZIARA "USWAZI"



Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akiwasili katika Kata ya Manzese (uswahilini) kwaajili ya ziara ya kuangalia Maendeleo ya wakazi wanaoendeleza makazi yao baada ya kupatiwa mikopo, kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Benki ya Azania Ngd. Charles G.Singili, benki yake inatoa pia mikopo kwa wajasiriamali na wananchi kwa lengo la kuyaendeleza makazi yao Jumatatu 23.07.2012 1200HOURZ

Mama, Profesa Tibaijuka Akipata maelekezo kutoka kwa Mama (Sada Juma Tagalile Mkazi wa manzese) Mjasiriamali aliyepata Mkopo wa kuboresha Nyumba yake- 23.07.2012

Profesa Akipata Maelezo Zaidi kutoka kwa mjumbe 23.07.2012.

Umakini wa Profesa Katika kusikiliza ndio kulivuta wakazi hawa wa Uswahilini na kumlaki Waziri Tibaijuka kwa Matumaini 23.07.2012 (Picha na D.M)

Hii ni Miongoni mwa Nyumba Zilizo katika Marekebisho, Jengo hilo linalotazamwa Ni la Bw.Twaha Ally Dima ambaye alipata Mkopo wa Milioni 4 tu kwaajili ya Kujenga Nyumba yake katika kata ya Manzese Uswazi

Hapa Mjumbe Akimuonyesha Moja ya Jengo la Biashara Lililojengwa Eneo Hilo la Manzese

Pongezi kwa Kumalizia Jengo la Biashara ama "Frame" ndivyo Mama Profesa anavyompa matumaini Mkazi wa manzese

waziri tibaijuka akisikiliza Maelekezo namna ambavyo wakazi wa Manzese wanavochangamkia mkopo wa kuboresha makazi

23.07.2012 Profesa akiwa Manzese Katika Ziara na hapa amesiama kusubiri mvua itulie aendelee na Ziara yake Uswahilini Huko

Ziara ikaendelea na hapa anatazama maendeleo ya Nyumba ya Mr.Twaha Ally Dima

Maelezo namana mkopo wa Milion ulivyopfanya kazi katika kupatikana Nyumba ya Mr.Twaha maelezo zaidi katika picha inayofuata.

Twaha Ally Abdalla Mkazi wa manzese akimuelezea kwa kina Profesa Namna alivyohangaika kupata Mkopo kwa miezi kumi na Hatimaye alifanikiwa kujenga Nyumba yake kama ambavyo inaonekana katika picha zilizotangulia

HABARI KWA KINA

 Neno “Uswahilini” ni la kawaida sana japo lilianza kutumika na linatumika kuonyesha na kuwaelezea watu wanaoishi maisha ya Chini.

Mpangilio mbovu wa makazi katika maeneo ya uswahili katika majiji mbalimbali huenda yakaigharimu serikali katika mpango wake wa kuboresha makazi unaoratibiwa na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi

Licha ya kuwepo hali hiyo Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka amewatoa hofu wananchi kuwa watafanikiwa kwa kufuata mpango wa kuboresha makazi huku wakitafuta namna ya kuboreha makazi hayo

 Katika hali ya Kuonyesha utofauti na Mawaziri wengine wa JK,  Profesa Tibaijuka amewasili katika kata ya Manzese Mvuleni na kutembelea nyumba kadhaa zilizoanza kuboreshwa katikati mwa kata hiyo yenye idadi kubwa ya makazi yasiyopangika

Mama Tiba, Akiwa hapo akatoa ufafanuzi endapo kuna mpango wowote wa kuyavunja makzi hayo ili kujenga ya kisasa zaidi na akatolea ufafanuzi suala hilo na kubwa akasema kuwa wameanzxa taratibu kwa kukata mti na kupanda mti na baadaye itajulikana nini cha kufanya

Wakazi mbalimbali wa maeneo hayo pamoja na kusifu uamuzi wa Waziri kufika katika maeneo hayo, bado wana hofu hasa katika kutegemea mkopo katika ujenzi wa makazi yao

Hata hivyo Wizara ya Profesa Tibaijuka bado ina kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wananeemeka na mradi wa kuboresha nyumba TAFSUS unaofanywa kwa kushirikiana na benki mbalimbali.
Kuhusiana na hali hiyo pamoj na mlolongo mrefu wa kupata mkopo 

 Bw. Twaha Ally Dima ni miongoni mwa wakazi waliofaidika na mpango huo kwa mkopo wa Milioni 4 tu huku Mkurugenzi wa Benki ya Azania Charles Singili akisema kuwa utaratibu wa nyumba ni mpya ila ana imani watanzania watauzoea utaratibu huo

Ziara ya Profesa Tibaijuka katika maeneo hayo yenye makazi duni yatuma ujumbe kwa wananchi kukubali mabadiliko katika makazi chini ya mkakati ulionzishwa na Waziri huyo wa sasa katika nyumba na makazi wakati akiwa Katika umoja wa mataifa-UN HABITAT


Waziri Tibaijuka Akifurahi Baada ya Twaha Ally Dima kumuuliza Waziri "unaonaje maeneo ya Huku Uswazi"? (picha zote na Dennis Mwasalanga)


1 comment:

  1. Kazi kwake mama Tiba cjui kama uswazi kutarekebika, nadhani Siri kali ilishachemka zamaniii

    ReplyDelete